11 Januari 2013 - 20:30

Baada ya kutembea zaidi ya kilometa 400 wapenzi wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) kukutana Mash`had kuomboleza na kuadhimisha kifo cha Mtukufu Mtume Muhammad(.s.a.w.w) na Imam Ridha(as).

ABNA- Wapenzi wa Ahlul Bayt(as) duniani kukusanyika Mash`had siku mbili za huzuni ambazo ni tarehe 28 na 29 Safar, Tarehe 28 Safar ni siku ulimwengu uligubikwa na huzuni kuondoka mbora wa viumbe Mtume Muhammad(s.a.w.w), Na kuacha pengo kubwa katika umma wa Kiislam.

Tarehe 29 Safar aidha ni siku ulimwengu uligubikwa na huzuni pia kwa kuuawa kishahidi mjukuu wa Mtume(s.a.w.w)  na wasii wake.

Siku hizi mbili ziliwakusanya wapenzi wa Ahlul Bayt(as) kuadhimisha vifo na shahada ya watukufu hao kwa kutuachia pengo ambalo kamwe haliwezi kuzibika, Ila la ajabu ni kwamba Waislam wamesahau siku hizi adhimu na kutofahamu siku aloaga dunia mbora wa viumbe Mtukufu Muhammad Ibn Abdillah(s.a.w.w).